• strict warning: Non-static method view::load() should not be called statically in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/views.module on line 879.
  • strict warning: Declaration of views_handler_filter::options_validate() should be compatible with views_handler::options_validate($form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/handlers/views_handler_filter.inc on line 589.
  • strict warning: Declaration of views_handler_filter::options_submit() should be compatible with views_handler::options_submit($form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/handlers/views_handler_filter.inc on line 589.
  • strict warning: Declaration of views_handler_filter_boolean_operator::value_validate() should be compatible with views_handler_filter::value_validate($form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/handlers/views_handler_filter_boolean_operator.inc on line 149.
  • strict warning: Declaration of views_plugin_row::options_validate() should be compatible with views_plugin::options_validate(&$form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/plugins/views_plugin_row.inc on line 135.
  • strict warning: Declaration of views_plugin_row::options_submit() should be compatible with views_plugin::options_submit(&$form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/plugins/views_plugin_row.inc on line 135.
  • strict warning: Non-static method view::load() should not be called statically in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/views.module on line 879.
  • strict warning: Non-static method view::load() should not be called statically in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/views.module on line 879.
  • strict warning: Declaration of views_plugin_style_default::options() should be compatible with views_object::options() in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/plugins/views_plugin_style_default.inc on line 25.

Simba 2- JKT RUVU 0

SIMBA leo imekuwa timu pekee katika Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu kushinda mechi zote mbili za ufunguzi baada ya kuifunga JKT Ruvu mabao 2-0 katika mchezo mkali uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi sita na kuwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Katika mchezo huo uliokuwa wa kusisimua, Simba ilipata mabao yake yote mawili kwenye kipindi cha pili baada ya timu zote kwenda sare katika kipindi cha kwanza.

Simba ilipata bao la kwanza kupitia kwa Amri Kiemba katika dakika ya 47 ya mchezo akiunganisha pasi ya kichwa ya Daniel Akuffo kutokana na mpira wa krosi uliopigwa na Mrisho Ngassa.

Dakika 20 baadaye, Haruna Moshi Boban aliipatia Simba bao la pili akimalizia kazi nzuri iliyofanywa tena na Ngassa.

Katika mchezo huo, Simba ilipata pigo baada ya mshambuliaji wake tegemeo lake, Emmanuel Okwi, kupewa kadi nyekundu katika kipindi cha kwanza baada ya mwamuzi kuona kwamba alimchezea rafu mchezaji wa JKT.

Simba itaingia tena uwanjani Jumapili ijayo kupambana na Ruvu Shooting Stars.

Simba iliwakilishwa na; Kaseja, Chollo, Maftah, Kapombe, Nyoso, Kiemba, Ngassa/Abdallah Juma, Mwinyi Kazimoto, Akuffo/Ramadhani Chomboh, Boban na Okwi.