• strict warning: Non-static method view::load() should not be called statically in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/views.module on line 879.
  • strict warning: Declaration of views_handler_filter::options_validate() should be compatible with views_handler::options_validate($form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/handlers/views_handler_filter.inc on line 589.
  • strict warning: Declaration of views_handler_filter::options_submit() should be compatible with views_handler::options_submit($form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/handlers/views_handler_filter.inc on line 589.
  • strict warning: Declaration of views_handler_filter_boolean_operator::value_validate() should be compatible with views_handler_filter::value_validate($form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/handlers/views_handler_filter_boolean_operator.inc on line 149.
  • strict warning: Declaration of views_plugin_row::options_validate() should be compatible with views_plugin::options_validate(&$form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/plugins/views_plugin_row.inc on line 135.
  • strict warning: Declaration of views_plugin_row::options_submit() should be compatible with views_plugin::options_submit(&$form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/plugins/views_plugin_row.inc on line 135.
  • strict warning: Non-static method view::load() should not be called statically in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/views.module on line 879.
  • strict warning: Non-static method view::load() should not be called statically in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/views.module on line 879.
  • strict warning: Declaration of views_plugin_style_default::options() should be compatible with views_object::options() in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/plugins/views_plugin_style_default.inc on line 25.

Simba mabingwa Banc ABC Sup8r

SIMBA imeendeleza utamaduni wake wa kutwaa kila kombe linaloanzishwa hapa nchini baada ya leo kuifunga Mtibwa ya Morogoro kwa mabao 4-3 na kutwaa Kombe la Banc ABC SUP8R.

Pambano hilo la fainali litakuwa miongoni mwa fainali tamu zaidi kuwahi kuchezwa katika Uwanja Mpya wa Taifa jijini Dar es Salaam na Mtibwa ilirejesha mara tatu mabao iliyofungwa na Simba kabla ya kufungwa la nne katika dakika 30 za nyongeza.

Shujaa wa Simba katika pambano hilo alikuwa mfungaji bora wa michuano hiyo, Edward Christopher Shija, ambaye alifunga mabao matatu " Hat Trick" katika pambano hilo kali na la kusisimua.

Christopher ambaye anafahamika zaidi kwa jina la Edo, alifunga mabao mawili katika muda wa kawaida na bao la mwisho alilifunga katika dakika 30 za mwisho.

Mfungaji wa bao lingine la Simba, Haruna Chanongo, yeye alifunga bao la tatu ambalo wengi wa waliokuwamo uwanjani waliamini lingekuwa la ushindi lakini Mtibwa wakarudisha dakika 10 kabla ya mpira kumalizika.

Kutokana na ushindi huo, Simba imepata zawadi ya Sh milioni 40.