• strict warning: Non-static method view::load() should not be called statically in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/views.module on line 879.
  • strict warning: Declaration of views_handler_filter::options_validate() should be compatible with views_handler::options_validate($form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/handlers/views_handler_filter.inc on line 589.
  • strict warning: Declaration of views_handler_filter::options_submit() should be compatible with views_handler::options_submit($form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/handlers/views_handler_filter.inc on line 589.
  • strict warning: Declaration of views_handler_filter_boolean_operator::value_validate() should be compatible with views_handler_filter::value_validate($form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/handlers/views_handler_filter_boolean_operator.inc on line 149.
  • strict warning: Declaration of views_plugin_row::options_validate() should be compatible with views_plugin::options_validate(&$form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/plugins/views_plugin_row.inc on line 135.
  • strict warning: Declaration of views_plugin_row::options_submit() should be compatible with views_plugin::options_submit(&$form, &$form_state) in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/plugins/views_plugin_row.inc on line 135.
  • strict warning: Non-static method view::load() should not be called statically in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/views.module on line 879.
  • strict warning: Non-static method view::load() should not be called statically in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/views.module on line 879.
  • strict warning: Declaration of views_plugin_style_default::options() should be compatible with views_object::options() in /home/simba10/public_html/sites/all/modules/views/plugins/views_plugin_style_default.inc on line 25.

Bao la Boban ni la kimataifa

KOCHA Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic, amesema bao alilofunga mshambuliaji wake, Haruna Moshi Boban, kwenye mechi dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), lina hadhi ya kimataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya pambano hilo, Cirkovic alisema bao la namna ile hufungwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa wa soka na pia kwenye mechi kubwa.

"Bao kama lile unaweza tu kuliona kwenye michuano mikubwa kama ya Euro au Kombe la Dunia. Ni wachezaji wachache sana wanaweza kufunga mabao ya namna ile. Boban amedhihirisha kwamba ni mchezaji mkubwa kwa kuweza kufunga bao lile,' alisema.

Boban alifunga bao hilo kwa kuunganisha moja kwa moja krosi iliyopigwa kutoka upande wa kulia wa lango la Vita na mchezaji mwenzake Mussa Mudde.

Pasi hiyo ya goli ilikuwa ya kwanza kutolewa na Mudde na tangu asajiliwe na Simba na Milovan amesema huo ni mwanzo wa mambo makubwa kutoka kwa mchezaji huyo wa Uganda.